array(0) { } Radio Maisha | Mwanafunzi aliyerejea nchini kutoka Uchina, kusalia katika chumba maalum, Mombasa

Mwanafunzi aliyerejea nchini kutoka Uchina, kusalia katika chumba maalum, Mombasa

Mwanafunzi aliyerejea nchini kutoka Uchina, kusalia katika chumba maalum, Mombasa

Mwanafunzi aliyerejea humu nchini kutoka Uchina Alhamisi wiki iliyopita, ataendelea kusalia kutengwa kwenye chumba maalum, wodi ya Rehemtullah katika Hospitali ya Rufaa ya Coast jijini Mombasa hadi matokeo ya sampuli za damu yake zilizopelekwa Afrika Kusini yatakapotolewa wiki ijayo.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka ishirini na miwili mkazi wa Senti Kumi, Likoni alitengwa kwenye chumba hicho tangu Ijumaa wiki hiyo akikisiwa kuathiriwa na Virusi vya Corona baada ya kudaiwa kulalamikia maumivu ya kifua na matatizo ya kupumua.

Idara ya Afya kwenye Kaunti hiyo imesema hali ya mwanafunzi huyo imeimarika japo hawezi ruhusiwa kutoka kwenye chumba hicho hadi pale itakapothibitishwa kama ameathiriwa na virusi hivyo au la.

Idara hiyo imesisitiza kuwapo kwa mikakati kabambe ya kuzuia virusi hivyo kusambaa kwa wakazi endapo mwanafunzi huyo atapatikana ameathiriwa na virusi hivyo vya Corona.

Ikumbukwe matokeo ya sampuli za damu ya mwanafunzi huyo yaliyotolewa Jumapili iliyopita kutoka kwa maaraba ya serikali jijini Nairobi yalibainisha kwamba  hajaathiriwa na Corona.

Mwanafunzi huyo anasomea taaluma ya Utabibu katika Chuo kikuu cha Guangzhou Southern University nchini Uchina na anadaiwa kuanza kulalamikia maumivu ya kifua na matatizo ya kupua alipokuwa huko.