array(0) { } Radio Maisha | Wafanyakazi wa Shirika la Habari la Standard wamuomboleza, Moi

Wafanyakazi wa Shirika la Habari la Standard wamuomboleza, Moi

Wafanyakazi wa Shirika la Habari la Standard wamuomboleza, Moi

Shirika la Habari la Standard, limefanya hafla ya kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Pili Hayati Daniel arap Moi katika Makao Makuu ya shirika hilo jijini Nairobi.

Wafanyakazi wa Shirika la Standard, wamekongamano mapema leo na  kujumuika na Wakenya wa matabaka mbalimbali kuomboleza kifo cha Moi ambaye alifariki dunia Jumanne.

Wafanyakazi wakiongozwa na Afisa Mkuu Mtendaji  Orlando Lyomu, wamechukua dakika moja ya kimya kuomwomboleza shujaa ambaye mchango wake umeoneka nchini vile vile nje ya taifa hili.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo Orlando amemtaja Moi kuwa kiongozi aliyepigania amani, umoja, ustawi wa Kenya na kukuza uhusiano bora kati ya Kenya na mataifa ya Bara la Afrika na zaidi.

Orlando aidha amemsifia Rais huyo mstaafu, na kumtamja kuwa nguzo ya elimu bora nchini baada ya kuanzisha Mfumo wa Elimu wa 8-4-4, na kuwa kielelezo cha utunzaji wa mazingira miongoni mwa mambo mengine muhimu aliyoyatekeleza.

Mkurugenzi huyo vilevile , ametoa changamoto kwa kila mmoja kuiga mfano wa Moi ambaye aliweka kipau mbele maslahi ya Wakenya.

Moi atazikwa Jumatano wiki ijayo nyumbani kwake Kabarak, kwenye Kaunti ya Baringo.