array(0) { } Radio Maisha | Rais aagiza bendera kupeperushwa nusu mlingoti kwa maombolezo ya Moi

Rais aagiza bendera kupeperushwa nusu mlingoti kwa maombolezo ya Moi

Rais aagiza bendera kupeperushwa nusu mlingoti kwa maombolezo ya Moi

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza kupeperushwa kwa bendera nusu mlingoti kwa heshima ya Rais Mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi ambaye amefariki dunia katika Hospitali ya Nairobi.

Kupitia taarifa rasmi kwa vyombo vya habari, Uhuru ameagiza bendera za Kenya katika ofisi za ubalozi wa Kenya kote duniani, kambi za polisi na za kijeshi, na taasisi za umma zipeperushwe nusu mlingoti hadi mwendazake atakapozikwa.

Aidha, katika taarifa hiyo, uhuru ametangaza kipindi cha kuomboleza kwa taifa kuanzia leo hadi pale atakapozikwa katika mazishi yatakayokuwa ya kitaifa.

Wakati uo huo, amamtaja Moi kuwa kiongozi aliyechangia pakubwa kuimarika kwa demokrasia ya vyama vingi na kuwa mzalendo aliyeondoka madarakani kwa amani pamoja na kuiwakilisha Kenya katika mikutano mbalimbali ya kimataifa nchini na ughaibuni.

Mwili wa marehemu umehamishwa hadi Hifadhi ya Maiti ya Lee, mita chache tu kutoka Hospitali hiyo huku ulinzi mkali wa maafisa wa polisi ukiripotiwa kwenye barabara zinazoelekea maeneo hayo.