array(0) { } Radio Maisha | Mzee Daniel Arap Moi aaga dunia

Mzee Daniel Arap Moi aaga dunia

Mzee Daniel Arap Moi aaga dunia

Taifa zima linaomboleza kifo cha Rais Mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi. Mzee Moi aliaga dunia saa 5. 20am tarehe 4/2/2020 katika hospitali na Nairobi Hospital.

Tangazo hilo lilitolewa mapema na Rais Uhuru Kenyatta ambaye amesema kwamba marehemu alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi.

Rais huyo mstaafu amekuwa akitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa kipindi cha miaka kadhaa licha ya kuarifiwa kuwa buheri wa afya wakati na baada ya utawala wake wa miaka 24.

Moi aliwahi kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake katika Hospitali ya Aga Khan mwaka 2017 baada ya kulalamikia maumivu yaliyotokana na ajali ya barabarani mwaka 2006.

Mwezi Machi mwaka 2018, mwanawe Gideon Mou na daktari wake David Silverstein waliandamana naye hadi nchini Israel katika safari waliotaja kuwa ya kawaida ya kukaguliwa goti lake. Mwishoni mwa mwaka 2018, Moi alilazwa katika Hospitali ya Nairobi kwa ukaguzi zaidi kabla ya kuruhusiwa kwenda myumbani baada ya siku kadhaa.

Marehemu ambaye alifahamika kwa jina Profesa wa siasa, atakubukwa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali wakiwemo wanasiasa nyumbani kwake Kabarak. Miongoni mwao wakiwa Rais Uhuru Kenyatta, mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir, Magavana mbalimbali, na Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli miongoni mwa wengine. Rais Mstaafu  atakumbukwa kauli mbalimbali ya ushauri kwa viongozi wa Kenya na Wakenya kwa ujumla.