array(0) { } Radio Maisha | Bodi ya kudhibiti filamu KFC yaonya magari kuhusu mijadala ya ngono

Bodi ya kudhibiti filamu KFC yaonya magari kuhusu mijadala ya ngono

Bodi ya kudhibiti filamu KFC yaonya magari kuhusu mijadala ya ngono

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Kudhibiti Filamu KFCB,Ezekiel Mutua ameonya magari yanayo beba wanafunzi kutosikiza stesheni nne nchini kwani asilimia kubwa ya mijadala yao inahusisha ngono.

Mutua amesema hayo akitoa onyo kuhakikisha zinachukua leseni itakayogharimu shilingi elfu mbili kila mwaka ya kuwaruhusu kuweka picha au video katika magari hayo.

Hatua hii inajiri baada ya madai kuwa baadhi ya magari ya umma huweka picha au video za ponografia, akisisitiza kuwa KFCB itadhibitisha picha zote na grafitti kabla kuwekwa katika magari. Mutua amesema kuwa magari yanayovunja sheria hiyo ni ya barabara za Ngong, Mombasa, Lang’ata, Thika na Magadi.

Vilevile Mutua amefurahishwa na hatua ya Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai kutangaza kuanza msako wa magari hayo.

Ametoa onyo hilo kwa vyama vya ushirika na mamba akisema watakao vunja sheria hizo watapigwa faini ya shilingi laki moja au kifungo cha miaka mitano.