array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa wawili wa wizi watekelezwa Mombasa

Washukiwa wawili wa wizi watekelezwa Mombasa

Washukiwa wawili wa wizi watekelezwa Mombasa

Washukiwa wawili wa wizi eneo la Likoni katika Kaunti ya Mombasa wameteketezwa kiasi cha kutotambuliwa na wahudumu wa bodaboda  baada ya jaribio lao la kuiba pikipiki ya muhudumu mmoja kutibuka.

Wawili hao wenye umri wa kati ya miaka ishirini na miwili na ishirini na mitano wameteketezwa mwendo wa saa kumi asubuhi katika mtaa wa Jamsa Feri.

Kamanda wa Polisi wa Likoni Jane Munyoki amesema kwamba wawili hao na mwenzao ambaye amefanikiwa kutoroka na majeraha walijifanya abiria waliotaka kubebwa kwa pikipiki.

Baadae watatu hao ambao walikuwa wamejihami kwa panga wamemshurutisha mhudumu huyo kwa lazima kuwaachia pikipiki yake hali iliyomlazimu kupiga kamsa iliyowavutia wahudumu wenzake.

Wahudumu wa bodaboda waliojawa na gadhabu wamewatekeza hadi kuwauwa washukiw kwa kutumia mafuta ya petroli huku mmoja kati ya watatu hao akitoroka.

Munyoki amesema kwamba msako wa kumtia mbaroni mshukiwa aliyefanikiwa kutoroka unaendelea.

Mili ya wawili hao imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Coast General.