array(0) { } Radio Maisha | Serikali kuwekeza zaidi katika Idara ya Polisi

Serikali kuwekeza zaidi katika Idara ya Polisi

Serikali kuwekeza zaidi katika Idara ya Polisi

Serikali itaendelea kuwekeza katika Idara ya Polisi ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake inavyostahili, amesema Rais Uhuru kenyatta.

Akizungumza baada ya kufungua rasmi Kanisa la Maafisa wa Kitengo cha Kukabili Ghasia  GSU mjini Ruiru, Kaunti ya Kiambu, Rais Kenyatta amesema viongozi wa kidini wanapotimiza mahitaji ya kiroho kwa maafisa wa polisi, Serikali itaendelea kutoa usaidizi kuwawezesha kutekeleza wajibu wao kwa uweledi.

Rais amewapongeza wote waliochangia ujenzi wa kanisa hilo jipya, huku akisema litatimiza mahitaji ya kiroho kwa maafisa wa polisi pamoja na familia zao kwenye kambi ya GSU ya Ruiru.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dakta Fred Matiang’i amemhakikishia Rais kwamba Idara ya Polisi haitamfeli katika huduma kwa Wakenya. 

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi Eliud Kinuthia, Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai na Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Edward Mbugua miongoni mwa maafisa wakuu serikalini.