array(0) { } Radio Maisha | Sitashurutishwa kumuunga yeyote mkono 2022 - Rais Kenyatta

Sitashurutishwa kumuunga yeyote mkono 2022 - Rais Kenyatta

Sitashurutishwa kumuunga yeyote mkono 2022 - Rais Kenyatta

Kwa mara nyingine Rais Uhuru Kenyatta amewataka viongozi kutomshinikiza kumuunga yeyote mkono wakati wa uchaguzi mkuu ujao, mwaka 2022.

Akizungumza kwa lugha ya Kikuyu katika uwanja wa Wang'uru alipowakabidhi wanunuzi wa zao la mchele shilingi milioni mia sita hamsini, Rais Kenyatta amesema kuwa kwa sasa yupo uongozini hadi wakati hatamu yake itakapomalizika.

Rais Kenyatta aidha ameeleza kuwa kwa sasa jukumu lake ni kuwaunganisha wananchi na wakati wa uchaguzi ukifika, wananchi wenyewe ndio watakaoamua.

Akiashiria suala la kung'atuliwa mamlakani kwa aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, rais ametoa onyo kwa viongozi wanaojihusisha na ufisadi kuwa hawatasazwa.


Kuhusu ununuzi mchele, kiongozi wa nchi ametoa agizo la kununuliwa kwa mpunga kwa bei ya shillingi themanini na tano tofauti na bei ya sasa ya shilingi sitini na tano.

Viongozi waliokuwa kwenye hafla hiyo ni pamoja na Gavana Ann Mumbi, Mwakilishi wa Kike Wangui Ngirici, Seneta Charlses Kibiru pamoja na wengine.