array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa Ukambani wapendekeza kubuniwa kwa Kaunti ya Mwingi

Viongozi wa Ukambani wapendekeza kubuniwa kwa Kaunti ya Mwingi

Viongozi wa Ukambani wapendekeza kubuniwa kwa Kaunti ya Mwingi

Viongozi wa Ukambani wameunga mkono pendekezo la kubuniwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu na manaibu wake wawili.

Katika maazimio yaliosomwa na Gavana wa Makueni, Profesa Kivutha Kibwana viongozi hao wanapendekeza kupanuliwa kwa mfumo wa uongozi ili kuhakikisha usawa.

Viongozi aidha wamependekeza seneti kupewa nguvu ili kufanikisha ugatuzi. Pia wanataka mawaziri kuteuliwa kutoka viongozi waliochaguliwa na ambao hawakuchaguliwa kwa lengo la kufanikisha utendakazi wao serikalini.

Aidha, wamependekeza Kaunti ya Kitui kugawanywa kutokana na ukubwa wake, huku wakita Mwingi kuwa kaunti kivyake.

Vilevile wamependekeza Mamlaka ya Uwekezaji Nchini, KIA kushirikiana na kaunti ili kufanikisha miradi ya maendeleo. Suala la ardhi pia limependekezwa ambapo ardhi za umma zinapaswa kurejeshwa kwa wananchi baada ya kukamilika kwa mkataba.

Wakati uo huo, suala la viwanda limezungumziwa kwa kina ambapo wito umetolewa kwa serikali kuvifufua viwanda vyote kwa lengo la kuimarisha sekta hiyo.

Maazimio hayo yamewasilishwa kwa Kinara wa ODM, Raila Odinga.