array(0) { } Radio Maisha | Mahakama yatupilia mbali ombi la Waititu kupinga uapisho wa Nyoro

Mahakama yatupilia mbali ombi la Waititu kupinga uapisho wa Nyoro

Mahakama yatupilia mbali ombi la Waititu kupinga uapisho wa Nyoro

Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu amepata pigo baada ya Mahakama ya Juu kutupilia mbali ombi lake la kutaka  kusitisha uapisho wa Naibu Gavana wa kaunti hiyo Dkt. James Nyoro.

Waititu alikuwa amewasilisha kesi mahakamani akitaka shughuli ya kumwapisha Nyoro isitishwe ili kuruhusu kesi aliyowasilisha kupinga kubanduliwa kwake kusikilizwa na kuamuliwa.

Hata hivyo, Jaji Weldon Korir amemwagiza Waititu kufika mahakamani Jumatatu mbele ya Jaji James Makau ili kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Haya yanajiri huku viongozi wa Kiambu wakifika katika  ofisi ya kaunti kwenye hafla ya kumwapisha Nyoro kuwa Gavana mpya wa kaunti hiyo