array(0) { } Radio Maisha | KQ yasitisha safari za ndege kutoka Uchina kwa sababu ya Corona

KQ yasitisha safari za ndege kutoka Uchina kwa sababu ya Corona

KQ yasitisha safari za ndege kutoka Uchina kwa sababu ya Corona

Shirika la Ndege la Kenya Airways, limesitisha safari zake kuelekea jijini Guangzhou, Uchina kufuatia kusambaa kwa Virusi vya Corona.

Katika taarifa kwa vyombo vya Habari Kenya Airways, hata hivyo imesema itaendelea na safari zake kuelekea Bankok, Thailand. Shirika hilo limesema litaendelea na mazungumzo na Waziri wa Afya na Wizara ya Mashauri ya Nchi za kigeni kuhusu suala hilo.

Hatua hii, imejiri siku moja tu baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Ndege kutishia kugoma kulishinikiza KQ kusitisha safari zake kuelekea Uchina.

Wakati uo huo, Ubalozi wa Uchina nchini umesema utashirikiana na kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo hadi humu nchini.

Tayari Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza Virusi vya Corona kuwa Janga la Kimataifa la Dharura la Afya.

Kufikia sasa WHO imesema idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia kusambaa kwa Corona ni 218 huku visa 98 vikiripotiwa nje ya Uchina.