array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta asema hatatikisika katika azma ya kuwahudumia Wakenya

Rais Kenyatta asema hatatikisika katika azma ya kuwahudumia Wakenya

Rais Kenyatta asema hatatikisika katika azma ya kuwahudumia Wakenya

"Sitaogopa wala kutikisika katika lengo la kuwaunganisha Wakenya.''

Ndiyo kauli ya Rais Uhuru Kenyatta akisisitiza kwamba hatayumbishwa na yeyote katika mpango wa kudumisha umoja miongoni mwa wananchi.

Akizungumza katika eneo la Salgaa, Kaunti ya Nakuru wakati wa kuzindua Kiwanda cha Saruji cha National Cement, Rais Kenyatta amesema taifa hili linaweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo iwapo viongozi watajiepusha na siasa za mwaka wa 2022.

Licha ya ushiriano wake na Kinara wa ODM, Raila Odinnga kuibua migawanyiko miongoni mwa wanasiasa, Kenyatta amesema hatalegeza kamba ya kuendeleza ushirikiano huo liwe liwalo.

Aidha, Rais amekariri wito wake kwa viongozi walioko serikalini kukoma kufanya siasa ili kuwatumikia wananchi.Kuhusu uzinduzi wa Kiwanda cha National Cement, Rais amesema shughuli hiyo inawiana na ajenda nne kuu za kufanikisha maendeleo.

Hata hivyo, Rais amesema utawala wake utaendelea kushughukilia jinsi ya kuimarisha uchumi wa taifa licha ya sekta mbalimbali kukumbwa na changamoto za kifedha.