array(0) { } Radio Maisha | Jane Kiano ametajwa kuwa
Jane Kiano ametajwa kuwa

''Msinibandue kwa sababu ya kesi ya ufisadi inayonikabili mahakamani.''

Ndiyo kauli ya Gavana wa Kiambu, Ferdnand Waititu akiyapuuza madai ya ufisadi yaliyoibuliwa dhidi yake na wawakilishi wadi wa Bunge la Kaunti ya Kiambu wakati wa kujadili hoja ya kumbandua.

Akizungumza wakati wa kikao maalumu cha seneti cha kuamua hatma yake, Waititu amesema wawakilishi wadi walipuuza haki za mshukiwa katika kesi yoyote na hivyo kumbandua kana kwamba tayari mahakama ilikuwa imempata na kosa na ufisadi.

Kuhusu madai ya kutumia mamlaka yake kupora fedha za umma kwa kuweka katika akaunti za mkewe na binti yake, Waititu amejitetea akisema madai hayo ni propaganda.

Hata hivyo Waititu amesema iwapo familia yake ina mashtaka ya kujibu inafaa idara za uchunguzi ziwawajibishe wanaohusika badala ya kumhusisha kwa kisingizo cha kuwa gavana.

Hata hivyo mawakili wa Bunge la Kaunti ya Kiambu wamesema kuna ushahidi wa kutosha kuthibitihsa madai yaliyoibuliwa dhidi ya Waititu.

Miongoni mwa madai yanayomkumba gavana Waititu ni ukiwamo ufisadi, utumiaji mbaya wa kiofisi, unyakuzi wa ardhi, kuajiri wafanyakazi kinyume na sheria, utumiaji wa fedha za kaunti kuliko asimilia 35 inayokubalika kisheria na ukiukaji wa katiba katika uongozi wake.

Kikao hicho kilianza saa tano baada ya Spika wa Seneti Ken Lusaka kumwagiza karani wa bunge hilo kusoma sababu zilizotumiwa na Bunge la Kiambu katika kumbadua Waititu mwezi uliopita.

Waititu anawakilishwa na mawakili kadhaa wakiwamo Peter Wanyama na Ng'ang'a Mbugua ambapo kikao hicho kinatarajiwa kuendelea saa nane.

Juma lililopita, Masenata walipiga kura ya kutaka hoja ya kubanduliwa kwa Gavana Waititu ijadiliwe na maseneta wote wala si kamati maalumu ya maseneta kumi na mmoja.\Msinibandue kwa sababu ya kesi ya ufisadi inayonikabili mahakamani.

Ndiyo kauli ya Gavana wa Kiambu, Ferdnand Waititu akiyapuuza madai ya ufisadi yaliyoibuliwa dhidi yake na wawakilishi wadi wa Bunge la Kaunti ya Kiambu wakati wa kujadili hoja ya kumbandua.

Akizungumza wakati wa kikao maalumu cha seneti cha kuamua hatma yake, Waititu amesema wawakilishi wadi walipuuza haki za mshukiwa katika kesi yoyote na hivyo kumbandua kana kwamba tayari mahakama ilikuwa imempata na kosa na ufisadi.

Kuhusu madai ya kutumia mamlaka yake kupora fedha za umma kwa kuweka katika akaunti za mkewe na binti yake, Waititu amejitetea akisema madai hayo ni propaganda.

Hata hivyo Waititu amesema iwapo familia yake ina mashtaka ya kujibu inafaa idara za uchunguzi ziwawajibishe wanaohusika badala ya kumhusisha kwa kisingizo cha kuwa gavana.

Hata hivyo mawakili wa Bunge la Kaunti ya Kiambu wamesema kuna ushahidi wa kutosha kuthibitihsa madai yaliyoibuliwa dhidi ya Waititu.

Miongoni mwa madai yanayomkumba gavana Waititu ni ukiwamo ufisadi, utumiaji mbaya wa kiofisi, unyakuzi wa ardhi, kuajiri wafanyakazi kinyume na sheria, utumiaji wa fedha za kaunti kuliko asimilia 35 inayokubalika kisheria na ukiukaji wa katiba katika uongozi wake.

Kikao hicho kilianza saa tano baada ya Spika wa Seneti Ken Lusaka kumwagiza karani wa bunge hilo kusoma sababu zilizotumiwa na Bunge la Kiambu katika kumbadua Waititu mwezi uliopita.

Waititu anawakilishwa na mawakili kadhaa wakiwamo Peter Wanyama na Ng'ang'a Mbugua ambapo kikao hicho kinatarajiwa kuendelea saa nane.

Juma lililopita, Masenata walipiga kura ya kutaka hoja ya kubanduliwa kwa Gavana Waititu ijadiliwe na maseneta wote wala si kamati maalumu ya maseneta kumi na mmoja.