array(0) { } Radio Maisha | Mwanafunzi atibiwa katika Hospitali ya KNH kufuatia hofu ya ugonjwa wa Corona

Mwanafunzi atibiwa katika Hospitali ya KNH kufuatia hofu ya ugonjwa wa Corona

Wanafunzi raia wa Kenya wanaosomea jijini Wuhan, Uchina wamelalamikia jinsi serikali inavyoshughulikia mahitaji yao wakati ambapo virusi vya Corona vinaendelea kusambaa nchini humo.

Kupitia mtandao wa Twitter  wanafunzi hao kupitia alama #KenyansInWahun, wamesema hakuna mawasiliano yoyote na Ubalozi wa Kenya jijini Beijing kuhusu afya na usalama wao.

Corenelius Mulili ambaye ni miongoni mwa wanafunzi hao amesema hali inaendelea kuwa ngumu zaidi kwa kuwa maduka na maeneo ya kuuza vyakula yamefungwa huku wakitakiwa kusalia nyumbani maafisa wa afya wakiendelea na uchunguzi.

Aidha Rono Kipkorir amesema kwa muda wa wiki mbili sasa tangu virusi hivyo vilipotangazwa, hakuna lolote ambalo Ubalozi wa Kenya umewafanyia.

Haya yanajiri huku Wizara ya Masuala ya Nchi za Kigeni hapa Jijini Nairobi, ikiwashauri raia wake wanaoishi Uchina kutosafiri kuelekea jijini Wahun, Hubei baada ya virusi hivyo kuzuka na kuenea.

Tayari watu zaidi ya mia moja wamethibitishwa kufariki dunia huku wengine zaidi ya elfu nne wakiambukizwa virusi hivyo.

Aidha Ujerumani imekuwa nchi ya hivi karibuni kuripoti kisa kimoja cha virusi hivyo.