array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta na Ruto wafanya kikao kwa zaidi ya saa tano

Rais Kenyatta na Ruto wafanya kikao kwa zaidi ya saa tano

Rais Kenyatta na Ruto wafanya kikao kwa zaidi ya saa tano

Rais Uhuru Kenyatta jana walishiriki mazungumzo na Naibu wake William Ruto kwa zaidi ya saa tano huku suala la Mpango wa Upatanishi, BBI na utawala katika Chama cha Jubilee likitawala kikao hicho katika Ikulu ya Nairobi.

Inaarifiwa kwamba Rais ndiye aliyempigia simu Ruto akimtaka wakutane faraghani huku wandani wa wawili hao wakidokeza kwamba suala la uchaguzi wa vyeo mbalimbali katika chama cha Jubilee mwezi Machi mwaka huu vilevile lilijadiliwa kwa kina. Vilevile, kuzuiliwa kuingia ofisini kwa Magavana wa Kiambu Ferdinand Waititu na mwenzake wa Nairobi Mike Sonko lilijadiliwa.

Aidha, ajenda nne kuu za serikali lilighusiwa pamoja na mchango wa mabunge yote mawili katika kufanikisha maono ya serikali ikizingatiwa kwamba wabunge wanarejelea vikao vyao baada ya kipindi cha wiki mbili zijazo.

Mkutano huo uliong'oa nanga mwendo wa saa nne na dakika kumi na kukamilika saa tisa, ulijiri siku moja tu baada ya Uhuru kukutana na jamaa wa familia yake kwa zaidi ya saa nne kapo yaliyojadiliwa hayajawekwa wazi.