array(0) { } Radio Maisha | Seneti kujadili hatma ya Gavana Waititu ambaye alibanduliwa na wawakilishi wadi

Seneti kujadili hatma ya Gavana Waititu ambaye alibanduliwa na wawakilishi wadi

Seneti kujadili hatma ya Gavana Waititu ambaye alibanduliwa na wawakilishi wadi

Bunge la Seneti asubuhi hii linatarajiwa kuandaa kikao maalum ambacho kitabaini hatma ya Gavana wa Kiambu Ferdinard Waititu ambaye Bunge la Kaunti yake lilipitisha hoja ya kutokuwa na imani naye.

Spika wa Bunge hilo Ken Lusaka alichapisha katika gazeti rasmi la serikali vikao vya leo baada ya maseneta kwa pamoja kuafikiana kwamba suala hilo linastahili kujadiliwa bungeni humo na wala si kupitia kamati maalum ambayo ilipaswa kubuniwa.

Wiki iliyopita, Masenata walipiga kura ya kutaka hoja za kubanduliwa mamlakani kwa Gavana Waititu kujadiliwa na bunge zima na wala si kamati maalum huku Seneta Maalum Isaac Mwaura akisema kuwa gavana huyo ni mshukiwa wa ufisadi na anapaswa kuwajishwa.

Tayari Lusaka amethibitisha kupokea stakabadhi zilizoorodhesha sababu za klumbandua Gavana Waititu kutoka kwa Bunge la Kiambu ambalo linasisitiza kwamba lilifuata utaratibu ufaao katika uamuzi wake.

Ikumbukwe Wawakilishi Wadi sitini na watatu walipitisha hoja ya kumbandua Waititu mwezi uliopita kufuatia madai ya ufisasi, na ukiukaji wa katiba.