array(0) { } Radio Maisha | Serikali itatumia shilingi bilioni mia moja hamsini kakarabati barabara nchini.

Serikali itatumia shilingi bilioni mia moja hamsini kakarabati barabara nchini.

Serikali itatumia shilingi bilioni mia moja hamsini kakarabati barabara nchini.

Serikali itatumia shilingi bilioni mia moja hamsini kuendeleza na kurekebisha miradi ya barabara ambayo imekwama katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Uchukuzi, James Macharia amesema kuwa fedha hizo zitatolewa na Bodi ya Barabara Nchini, Kenya Roads Board kufikia mwezi wa tatu mwaka huu 2020.

Akizungumza wakati wa kikao na wanahabari jijini Kisumu, Macharia aidha amethibitisha kuwa changamoto za kifedha ndizo zimechelewesha kukamilika kwa miradi ya barabara, vilevile ukarabati wa mara kwa mara wa barabara za mashinani.

Kulingana naye, hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kusaini marekebisho ya mswada wa Bodi ya Barabara Nchini wa mwaka 2019, inaipa fursa serikali kufadhili mirdi ya ujenzi wa barabara iliyokwama.

Kuhusu ujenzi wa Bandari ya Kisumu, Macharia amesema ukarabati huo umefikia asilimia tisini na nane na kwamba utakamilika ndani ya wiki mbili zijazo kabla ya kufunguliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta na Mwakilishi Maalum wa Miundomsingi Barani Afrika Raila Odinga, jinsi ilivyopangwa hapo awali.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwaonya wasimamizi wa ujenzi wa bandari hiyo, akisema ukaguzi wa fedha zinazotumika katika shughuli hiyo utafanywa ili kubaini kiwango halisi kilichotumika ikilinganishwa na fedha zilizokadiriwa