array(0) { } Radio Maisha | Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dakta Fred Matiang'i leo hii amefanya mkutano na wakuu wa usalama kwenye Kaunti ya Garissa ili kujadili suala la utovu wa usalama kwenye eneo hilo.

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dakta Fred Matiang'i leo hii amefanya mkutano na wakuu wa usalama kwenye Kaunti ya Garissa ili kujadili suala la utovu wa usalama kwenye eneo hilo.

Matiang'i amesema serikali imeweka mikakati ili kuhakikisha suala la utovu wa usalama linakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Amesema polisi zaidi wametumwa kushika doria mpakani pa Kenya na Somalia ili kuhakikisha washukiwa wa Al Shabaab wanakabiliwa.

Amewashauri maafisa wa usalama kushirikiana na wakazi katika kuwakabili magaidi.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai unajiri majuma kadhaa baada ya walimu watatu, wanafunzi wanne na maafisa wawili wa Jeshi la Ulinzi, KDF kuuliwa katika kaunti hiyo kufuatia shambulio la kigaidi.

Shambulio hilo lilisababisha Tume ya Huduma za Walimu, TSC kuwapa likizo ya muda walimu wasiokuwa wenyeji wa eneo la Kaskazini Mashariki baada ya kulalamikia usalama wao