array(0) { } Radio Maisha | Jane Kiano ametajwa kuwa
Jane Kiano ametajwa kuwa

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha, ametoa wito kwa washikadau wa elimu nchini kushirikiana na serikali kufanikisha mpango wa mpito wa asilimia moja ya wanafunzi wanaojiunga na shule za upili.

Magoha amesema kuwa takriban wanafunzi laki moja wanaostahili kujiunga na shule za upili hawajajiunga na shule hizo, akiwataka maafisa wa elimu nyanjani kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanajiunga na shule hizo.

Profesa Magoha aidha, amesema kuwa asilimia 92 ya wanafanunzi ambao walifanya KCPE mwaka uliopita tayari wamejiunga na shule hizo huku akisema kuwa kampeni ambayo imekuwa ikiendelea kuwatafuta wanafunzi ambao hawajajiunga na shule za upili imezaa matunda ambapo wanafunzi laki moja unusu wamepatikana na kupelekwa shuleni.

Magoha ambaye ameongoza shughuli ya kuwatafuta wanafunzi hao, amesema mfumo wa asilimia mia moja lazima utafanikishwa akisisitiza kuwa hakuna mwanafunzi ambaye atafungiwa nje kwa ajili ya ukosefu wa karo.

Akizindua mpango wa nyumba hadi nyumba kuwatafuta wanafunzi hao mtaani Kibra wiki iliyopita,  Magoha alisema kuwa elimu ni mojawapo ya ajenda kuu ya serikali na ambayo lazima itekelezwa kikamilifu.

Waziri huyo akiwa ameandamana na Katibu wa Wizara ya Elimu, Dakta Belio Kipsang amewapeleka wanafunzi watatu katika shule za Moi Girls na Lang'ata High ambao walikuwa wamesalia nyumbani kwa ajili ya ukosefu wa karo.

Kwa mara nyingine, Magoha amewaonya walimu kuu dhidi ya kuwatuma nyumbani wanafunzi kufuatia ukosefu wa karo.


Waziri huyo vilevile amesema kuwa jumla ya kaunti 11 zikiongozwa na Murang'a zimefanikiwa kuwapeleka wanafunzi wote waliofanya KCPE mwaka jana kwenye shule za upili.