array(0) { } Radio Maisha | Ndege wa aina ya Osprey aliyetoka Finland kuja Kenya amekufa.

Ndege wa aina ya Osprey aliyetoka Finland kuja Kenya amekufa.

Ndege wa aina ya Osprey aliyetoka Finland kuja Kenya amekufa.

Ndege wa aina ya Osprey aliyetoka taifa la Finland kuja Kenya amekufa. Ndege huyo aliyepaa takribani kilomita elfu saba ana umri wa miaka minne alifika Kenya wikendi hii na kutua katika Mbuga ya Nairobi Mtaani Karen.

Uchunguzi ambao umefanywa na maafisa wa wanyama umebaini kwamba kifo cha ndege huyo kimesababishwa na mwendo mrefu, njaa vilevile kufeli kwa viungo vya mwili.

Msemaji wa Shirika la Huduma za Wanyamapori, KWS Paul Odoto ambaye ametangaza kifo cha Osprey amesema juhudi za maafisa wa KWS kumnusuru ziliambulia patupu.

Ijumaa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Utafiti katika shirika hilo, Dakta Patrick Omondi aliwaambia wanahabari kwamba ndege huyo angerejeshwa Finland baada ya matibabu..