array(0) { } Radio Maisha | Marekani inaunga mkono mpango wa upatanishi BBI

Marekani inaunga mkono mpango wa upatanishi BBI

Marekani inaunga mkono mpango wa upatanishi BBI

Serikali ya Marekani inaunga mkono mpango wa upatanishi BBI ili kuzipa serikali za kaunti mamlaka zaidi kupitia ugatuzi.

Balozi wa Marekani humu nchini Kyle McCarter ambaye yuko ziarani kwenye Kaunti ya Bungoma amesema kwamba Marekani itaendelea kupiga jeki mpango wa kuimarisha elimu ya kiufundi nchini kupitia vyuo anuwai chini ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti.

Kwa upande wake Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati, ametoa hakikisho kuwa Baraza la Magavana litahakikisha mjadala kuhusu mpango wa upatanishi BBI unaafikis malengo ya kuimarisha ugatuzi nchini.

Serikali ya Marekani kupitia ubalozi wake humu nchini inatathmini miradi inayofanywa kupitia ufadhili wa marekani ikiwemo sekta ya afya katika kaunti zote 47 nchini, Kaunti ya Bungoma ikiwa ya 34.