array(0) { } Radio Maisha | Baraza la Kukabili Ugonjwa wa HIV, linafanya kongamano Mombasa

Baraza la Kukabili Ugonjwa wa HIV, linafanya kongamano Mombasa

Baraza la Kukabili Ugonjwa wa HIV, linafanya kongamano Mombasa

Baraza la Kitaifa la Kukabili Ugonjwa wa HIV, NACC linafanya kongamano na viongozi wa kaunti zilizorekodi idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya HIV jijini Mombasa.

Gavana wa Homa Bay, Cyprian Owiti mmoja wa wanaohudhuria kongamano hilo amesema viongozi wa kaunti yake wamekuwa wakifanya uhamasisho kwa wakazi huku wahudumu wa bodaboda miongoni mwa washikadau wengine wakihusishwa pakubwa.

Gavana Owito aidha amewashauri wananchi kuvitembelea vituo vya afya ili kupimwa iwapo wameambukizwa virusi hivyo.

Naibu Gavana wa kaunti hiyo, Hamilton Orata kwa upande wake amewashauri vijana kujikinga kila wanaposhiriki ngono ili kupunguza maambukizi ya HIV.

Wakati uo huo, Mkurugenzi wa NACC, Ndung'u Kilongu amezishauri kaunti kutenga fedha ili kuwanufaisha waathiriwa wa ugonjwa huo. Kilongu hata hivyo amewapongeza magavana ambao tayari wamejitokeza katika vita dhidi ya maambukizi ya HIV na ugonjwa wa Ukimwi.