array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa Jubilee waunga mkono BBI kwa masharti

Viongozi wa Jubilee waunga mkono BBI kwa masharti

Viongozi wa Jubilee waunga mkono BBI kwa masharti

Viongozi mia moja sabini na watatu wa Chama cha Jubilee wameafikiana kuendelea kuunga mkono Mpango wa Upatanishi, BBI japo kwa masharti.

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti, Kipchumba Murkomen ambaye anaongoza kikao hicho, amekana kwamba kuna mipango ya kuendesha mikutano sambamba na ya BBI kwenye maeneo mbalimbali nchini. Murkomen amesema kwamba watashinikiza mikutano hiyo kuandaliwa kote nchini ili wananchi waweze kupaaza sauti zao.

Aidha, viongozi hao wameafikiana kwamba watachanga fedha za kugharimia shughuli za mikutano hiyo wakati itakapokuwa ikiandaliwa katika kaunti ambazo zinaongozwa na magavana wa mrengo wa Jubilee, bila kumlipa yeyote kwa ajili ya kuhudhuria.

Wakati uo huo, wameahidi kuhakikisha kwamba masuala yanayowahusu wananchi yanajadiliwa kwa kina ukiwamo mgao wa fedha za kaunti, uhuru wa idara ya mahakama na kadhalika.