array(0) { } Radio Maisha | Uchina yaweka mikakati ya kukabili virusi vya Corona

Uchina yaweka mikakati ya kukabili virusi vya Corona

Uchina yaweka mikakati ya kukabili virusi vya Corona

Wakurugenzi wa kampuni mbalimbali nchini Uchina wamewashauri wafanyakazi wao kufanyia kazi nyumbani ili kuepuka Virusi vya Corona ambavyo vimesababisha vifo vya watu themanini kufikia sasa huku wengine zaidi ya 2,700 wakiendelea kutibiwa.

Aidha, baadhi ya kampuni zimelazimika kuwatuma wafanyakazi kwa likizo ndefu, baadhi wakishauriwa kutofanya ziara ya kwenda katika mataifa mengine.

Jiji la Wuhan ambalo limeathiriwa zaidi tayari limethibitiwa, wananchi wakishauriwa kutotoroka chumbani hasa wakati wa upepo mkubwa. Hoteli ya Kimataifa ya Hotpot Chain Haidilao vilevile imetangaza kwamba itasitisha shughuli zake kwa muda ili kuepuka virusi hivyo.

Vilevile benki za UBS Group AG zimetoa ushauri kwa wateja wao kusalia nyumbani na badala yake kutoa pesa kwa kutumia simu zao.

Ikumbukwe kampuni za Hong Kong Exchanges na  Clearing Ltd, HKEX zilisitisha shughuli zake Jumatano wiki jana katika harakati za kuepuka Virusi vya Corona.

......................