array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa wanne wa uhalifu wamekamatwa Nairobi

Washukiwa wanne wa uhalifu wamekamatwa Nairobi

Washukiwa wanne wa uhalifu wamekamatwa Nairobi

Washukiwa wanne wa uhalifu wamekamatwa jijini Nairobi kufuatia tuhuma za kuwahangaisha wakazi wa mitaa ya Kilimani na Kileleshwa wakitumia pikipiki.

Washukiwa hao ambao ni Abdul Jafar, Derick Simani, Sadiq Mohamed na Hassan Musa Chepkoech walikamatwa jana jioni.

Kupitia mtandao wa Twitter, Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, DCI George Kinoti amesema maafisa wake walianzisha msako huo kufuatia ripoti za umma kwamba kuna watu waliokuwa wakitumia bodaboda kuwaibia, kuwapiga na hata kuwaua baadhi kwa kuwafyetulia risasi.

Bastola moja, baiskeli yenye nambari ya usajili KMFA 500Z, KMET 389K na nyingine mbili bila nambari za usajili zimepatikana. Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo hii.

Mwaka uliopita, makachero wa DCI waliwakamata washukiwa wengine waliokuwa wakiwahangaisha wakazi katika mitaa iyo hiyo.