array(0) { } Radio Maisha | Naunga mkono BBI wala si sera za Raila, asema Moses Kuria

Naunga mkono BBI wala si sera za Raila, asema Moses Kuria

Naunga mkono BBI wala si sera za Raila, asema Moses Kuria

"Iwapo kumuunga mkono Kinara wa ODM, Raila Odinga ni tiketi ya kuingia mbinguni, basi nimekubali kwenda jehanamu" Ndiyo kauli ya Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria ambaye aidha amewasuta wandani wa Raila kwa kuwashinikza washirika wa Naibu wa Rais, William Ruto kumwita Raila Baba.

Kuria amesema katika mkutano wa jana katika Bustani ya Mama Ngina jijini Mombasa, wandani wa Ruto awali walidhalilishwa wakiingia uwanjani humo kufuatia misimamo yao.

Amesema wakati mmoja alinyimwa kiti kwa madai ya kumkosea heshima Raila awali. Wakati uo huo, amemsuta Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Nairobi, Peter Imwatok kwa kumpokonya kofia yenye maandishi BBI.

Kuria amesema Mpango wa BBI unatumika katika kufanikisha siasa za mwaka wa 2022, na wote wanaomuunga mkono Raila wamejipanga kuunda muungano wa kisiasa ili kufanikisha azma ya kinara huyo kuingia ikulu.

Amesema anaunga mkono BBI lakini haungi mkono sera za Raila Odinga.