array(0) { } Radio Maisha | Baraza la Wahariri limesikitikia kuendelea kushambuliwa kwa wanahabari.

Baraza la Wahariri limesikitikia kuendelea kushambuliwa kwa wanahabari.

Baraza la Wahariri limesikitikia kuendelea kushambuliwa kwa wanahabari.

Baraza la Wahariri wa Vyombo vya Habari limesikitikia ongezeko la visa vya wanahabari kushambuliwaKatika barua iliyoandikiwa Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai wahariri hao wamelalamika kuwa maafisa wa polisi ambao wanajukumu la utumishi kwa wote ndio wanaowashambulia wanahabari.

Haya yanajiri baada ya wanahabari wanne kushambuliwa mwaka huu pekee. Tarehe 10 mwezi huu mwanahabari wa KTN NEWS Brian Obuya na wa Daily Nation Wanjohi Githae walishambuliwa na maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kilimani baada ya kukamatwa kwa Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria.

Tarehe 12 mwezi huu mwanahabari wa Inooro TV Robert Maina alishambuliwa katika Kituo cha Polisi cha Njoro alipokuwa katika maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton.

Kisha tarehe 13  katika Kaunti ya Mombasa mwanahabari wa Daily Nation Laban Walloga alishambuliwa na maafisa wa polisi alipokuwa katika maandamano ya wanaopinga usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya kisasa SGR.

Kisa cha hivi punde ni cha leo alfajiri ambapo mwanahabari wa Mbaitu FM amejeruhiwa kwa kukatwa kwa panga kwenye eneo la Tala Matungulu katika Kaunti ya Machakos.

Mwanahabari huyo kwa jina Boniface Wambua anaendelea kutibiwa katika Hospitali moja Mjini Tala. Hii hapa sauti yake akielezea uvamizi huo.