array(0) { } Radio Maisha | Mwanablogu Cyprian Nyakundi amekamatwa kwa tuhuma za ulaghai.

Mwanablogu Cyprian Nyakundi amekamatwa kwa tuhuma za ulaghai.

Mwanablogu Cyprian Nyakundi amekamatwa kwa tuhuma za ulaghai.

Makachero wa Idara ya Upelelezi DCI, wanaendelea kumhoji mwanablogu Cyprian Nyakundi na Emmanuel Nyamweya wakihusishwa na tuhuma za ulaghai.

Wawili hao wamenaswa saa moja iliyopita wakiwa katika harakati ya kupokea shilingi milioni moja  kutoka kwa mmoja wa waathiriwa wa ulaghai wao.

Kulingana na DCI,wawili hao walikuwa wameitisha kima cha shilingi milioni 17.5 ili kuondoa taarifa ya kumharibia jina mwathiriwa iliyokuwa imechapishwa kwenye tovuti ya mmoja wa washukiwa

Polisi wamefanikiwa kurejesha fedha hizo shilingi milioni moja huku washukiwa wakitarajiwa kufikisha kesho mahakamani, ambapo watafunguliwa mashtaka ya ulaghai na matumizi mabaya ya mtandao