array(0) { } Radio Maisha | Gavana Waititu apata pigo mahakamani

Gavana Waititu apata pigo mahakamani

Gavana Waititu apata pigo mahakamani

Mahakama ya Milimani imekataa kusitisha kesi ya ufisadi inayomkabili Gavana wa Kiambu, Fardinand Waititu anayetuhumiwa kuhusika na ufujaji wa shilingi milioni mia tano themanini na nane.

Waititu aliwasilisha ombi mahakamani la kutaka kesi dhidi yake kusitishwa kwa muda ili kumruhusu ahudhurie vikao vya Bunge la Seneti Jumanne tarehe ishirini na moja mwezi huu.

Katika uamuzi wake mapema leo, Hakimu Thomas Nzioki amesema Gavana Waititu amekosa kuwasilisha stakabadhi zinazoonesha kuwa Bunge la Seneti lilimwagiza kufika mbele yake.

Bunge la Seneti tayari limeitisha kikao maalum Jumanne wiki ijayo kujadili hatua ya Bunge la Kaunti ya Kiambu kumng'atua mamlakani Waititu kufuatia madai ya ufisadi.