array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta aahidi kuimarishwa kwa viti dhidi ya magaidi

Rais Kenyatta aahidi kuimarishwa kwa viti dhidi ya magaidi

Rais Kenyatta aahidi kuimarishwa kwa viti dhidi ya magaidi

Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa serikali itaendeleza operesheni kali dhidi ya mashambulio ya kigadi ili kuwapa Wakenya na raia wa kigeni usalama wa kutosha.

Kenyatta amesema kuwa hilo litaafikiwa kupitia mafunzo kwa vikosi vya usalama ili kuviwezesha kuwakabili magaidi wa Al Shabaab

Akizungumza wakati wa kikao na Wakuu wa Idara ya Usalama katika Ikulu ya Mombasa, Kenyatta amesema mafunzo hayo yatawalenga maafisa wanaohudumu katika maeneo yanaokumbwa na utovu wa usalama. Aidha amesema Tume ya Huduma za Polisi itafanyiwa mchujo , ikiwa njia mojawapo ya kuimairisha utendakazi wake kwa Wakenya

Rais vilevile, amesema serikali aidha imeweka mikakati ya kuzuia kufadhiliwa kwa magaidi wa Al Shabaab, huku akiwaonya wanaohusika katika kutoa ama kuchangia katika ufadhili wa makundi ya kigaidi nchini. Kenyatta amesema serikali itawaorodhesha watu hao hivi karibuni.

Wakati uo huo,  Kenyatta amesisitiza onyo kuhusu kuingizwa nchini kwa bidhaa za magendo hasa mipakani, akisema hali hiyo imewasaidia magaidi wa Ashabaa kupata ufadhili.

Kenyatta vilevile, imeagiza kutuzwa mara moja kwa maafisa wa polisi ambao wameonesha uchapaji kazi katika vitengo mbalimbali ikiwa njia mojawapo ya kuwapa motisha .

Rais  ameziagiza Tume ya Huduma za Umma, Tume ya Huduma za Polisi na Tume ya Kuratibu Mishahara ya Wanyakazi, kuweka mikakati ya kuwatuza polisi ambao wameng'aa kazini.