array(0) { } Radio Maisha | Mahakama yabatilisha uteuzi wa Mary Wambui kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Uajiri

Mahakama yabatilisha uteuzi wa Mary Wambui kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Uajiri

Mahakama yabatilisha uteuzi wa Mary Wambui kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Uajiri

Mahakama ya Uajiri na Leba imefutilia mbali uteuzi wa aliyekuwa Mbunge wa Othaya, Mary Wambui katika wadhifa wa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Uajiri Nchini.

Katika uamuzi ambao umetolewa muda mfupi uliopita mahakama imesema kwamba Wambui hajahitimu inavyohitajika kushikilia wadhfa huo.

Ikumbukwe Oktoba mwaka jana Hakimu wa Mahakama iyo hiyo ya Leba, Heleln Wasilwa alimzuia Wambui kutekeleza majukumu yoyote ya mamlaka hiyo hadi kesi iliyowasilishwa dhidi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Kesi ya kupinga uteuzi wake iliwasilishwa na wabunge vijana wakiongozwa na Seneta wa Nairobi Jonstone Sakaja, wakisema Wambui hana tajriba ya kutosha kielimu kushikilia wadhifa huo.

Aidha waliieleza mahakama kwamba matakwa ya anayeteuliwa katika wadhifa huo ni lazima yazingatie sheria za uajiri.