array(0) { } Radio Maisha | EACC yajiondolewa lawama kuhusu madai ya kutowajibikia vita dhidi ya ufisadi

EACC yajiondolewa lawama kuhusu madai ya kutowajibikia vita dhidi ya ufisadi

EACC yajiondolewa lawama kuhusu madai ya kutowajibikia vita dhidi ya ufisadi

Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC Twalib Mbarak amekashifu vikali madai kuwa EACC haijawajibika katika vita dhidi ya ufisadi akisema kuwa kati ya mwaka 20180-2019 kesi 78 za ufisadi ziliwasilishwa mahakamani miongoni mwao 51 zilitolewa uamuzi.

Vilevile Twali amesema kuwa EACC haitajihusishwa na vita vya ukoo katika maeneo ya Kaskazini Mashariki akisisitiza kuwa lengo la EACC ni kukabili ufisadi na kuwa hatakubali kutumiwa kumkamdamiza mtu kwa misingi ya vurugu za kikoo.

Amesema hayo baada ya kutia saini mkataba na Muungano wa mataifa ya Ulaya EU kuwapa mafunzo maafisaa wa tume hiyo katika vita dhidi ya ufisadi kwa kufanya uchunguzi wa kina na kukamatwa kwa wanaojihusisha na ufisadi.

Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC, Twalib Mbaruk amesema kuwa ushirikiano huo utasaidia pakubwa katika mikakati ya kurudisha mali inayomilikiwa kinyume na sheria.

Balozi wa EU, Simon Mordue amesema kuwa wamewekeza shilingi billioni 3 katika mpango huo, akipongeza EACC kwa juhudi walizoweka mwaka jana katika kuwakamata watu fisadi na kurudisha baadhi ya mali iliyomilikiwa kinyume na sheria.

Balozi huyo amepongeza hotuba ya Rais ya mapema wiki hii aliposema kuwa mwaka huu mikakati zaidi ya kuwakabili watu fisadi itawekwa.