array(0) { } Radio Maisha | Watu wanne wajeruhiwa katika ajali ya ndege Kajiado

Watu wanne wajeruhiwa katika ajali ya ndege Kajiado

Watu wanne wajeruhiwa katika ajali ya ndege Kajiado

Uchunguzi umeanzishwa kufuatia ajali ya ndege ambapo watu wanne wamejeruhiwa. Inaarifiwa ndege hiyo ya Kampuni ya Yellow Winga Air Services ilipata hitilafu na kulazimika kutua ghafla kwenye eneo la Mashuru Kaunti ya Kajiado.


Mkuu wa polisi wa eneo la Kajiado Stephen Nyakundi amesema watatu hao walipata tu majeraha madogo na wako katika hali nzuri.


Waliokuwa kwenye ndege hiyo wametambuliwa kuwa Peter Almendinger ambaye ni rubani na Russell, Paris na Susan ambao ni watalii