array(0) { } Radio Maisha | Chama cha Maendeleo ya Wanawake chaunga mkono mabadiliko katiba Baraza la Mawaziri

Chama cha Maendeleo ya Wanawake chaunga mkono mabadiliko katiba Baraza la Mawaziri

Chama cha Maendeleo ya Wanawake chaunga mkono mabadiliko katiba Baraza la Mawaziri

Chama cha Maendeleo ya Wanawake kinaunga mkono mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, amesema Mwenyekiti wa chama hicho Rahab Mwikali.

Akihutubu jijini Nairobi, Mwikali amesema mabadiliko hayo yaliofanywa na Rais Uhuru Kenyatta Jumatano wiki hii yanalenga kuboresha utendakazi katika serikali yake.

Mwikali aidha amewasihi wanasiasa kuwaheshimu viongozi wakuu serikalini na hata upinzani ili kupunguza joto la kisiasa nchini. Amesema viongozi wanapaswa kutafuta njia mwafaka ya kuwasilisha malalamiko yao kuhusu viongozi fulani badala ya kutumia matusi kila wanapokuwa majukwaani.

Kauli yake imetiliwa mkazo na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Zipporah Kittony ambaye amewashauri Wakenya kuweka kando tofauti zao na badala yake kuhubiri amani. Amesema hulka za viongozi kurushiana maneno huenda zikatumbukiza taifa hilo katika mapigano sawa na yalioshuhudiwa mwaka wa 2007.