array(0) { } Radio Maisha | Familia yaangamia kufuatia maporomoko ya ardhi Turkana

Familia yaangamia kufuatia maporomoko ya ardhi Turkana

Familia yaangamia kufuatia maporomoko ya ardhi Turkana

Baba, mama na mwanao wamefariki dunia katika Kijiji cha Mwasere Kaunti ya Taita Taveta baada ya nyumba yao kuporomoka usiku wa kuamkia leo.

Inaarifiwa nyumba hiyo imeporomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika maeneo mbalimbali ya Pwani.

Jumatatu wiki hii, Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga ilionya kwamba mvua kubwa itashuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi wiki hii.

Kupitia taarifa yake katika mtandao wa Twitter, Idara hiyo ilisema mvua kubwa itaandamana na juzi joto kati ya 12 na 26 katika Kaunti za Nyeri, Makindu, Nairobi, Garissa, Kisumu, Taita Taveta,  Narok, Lamu, Mombasa, Meru na Samburu.

Juma lililopita, idara hiyo ilisema kuwa mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha ingepungua.