array(0) { } Radio Maisha | Marekani yaipongeza Kenya kwa juhudi za kukabili ugaidi

Marekani yaipongeza Kenya kwa juhudi za kukabili ugaidi

Marekani yaipongeza Kenya kwa juhudi za kukabili ugaidi

Marekani imeipongeza Serikali ya Kenya kwa juhudi za kuendelea kuyakabili mashambulio ya kigaidi nchini.

Merekani imesisitiza kujitolea kwake kuisaidia Kenya kukabili suala hilo, wakati taifa linaadhimisha mwaka mmoja tangu shambulio la Dusit d2, kufanyika ambapo watu ishirini na mmoja waliuliwa.

Kupitia taarifa ya Ubalozi wake nchini, taifa hilo limesema litaendelea kuwapa mafunzo ya kijasusi polisi wa Kenya ikiwa njia mojawapo ya kuwakabili magaidi wa Al-Shabaab.

Marekani aidha imekashifu misururu ya mashambuli hayo, ikisema itatoa mchango wake kuwakabili magaidi wanaolenga kusambaratisha uchumi na maendeleo ya Afrika Mashariki.

Kundi hilo linalofungamana na Al-Qaeda, lilitekeleza shambulio la Dusitd2 huku Marekani ikivipongeza vikosi vya usalama nchini kwa ushirikiano uliofanikisha kuuliwa kwa magaidi hao .

Maadhimisho ya leo yanafanyika huku usalama ukiwa umeimarishwa jijini Nairobi na katika mkahawa huo kuzuia shambulio jingine baada ya maeneo la Lamu na Garissa kukumbwa na misururu ya mashambulio siku za hivi karibuni.

Magaidi wa Al Shabaab juma hili wameshambulia Shule ya Kamuthe katika Kaunti ya Garissa, ambapo walimu watatu waliuliwa na mmoja kujeruhiwa.