array(0) { } Radio Maisha | Kiunjuri asema hajasangazwa na hatua ya Rais Kenyatta kumsimamisha kazi

Kiunjuri asema hajasangazwa na hatua ya Rais Kenyatta kumsimamisha kazi

Kiunjuri asema hajasangazwa na hatua ya Rais Kenyatta kumsimamisha kazi

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mwangi  Kiunjuri amesema hajashangazwa na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kumsimamisha kazi. Akiwahutubia wanahabari, Kiunjuri amesema kwa muda amekuwa akipitia changamoto katika utendakazi wake ambazo familia yake inazifahamu huku akisema Rais alikuwa na uhuru wa kufanya uamuzi aliochukua.

Kiunjuri hata hivyo amesema anajivunia muda ambao amehudumu akisema Rais mwenyewe pia anatambua kuhusu kuimarika kwa sekta ya kilimo aliyoisimamia. Amemtakia Munya kila la kheri katika majukumu mapya aliyokabidhiwa.

Akiulizwa masuali na wanahabari, Kiunjuri hata hivyo amekataa kukiri iwapo kufutwa kwake kumechochewa kisiasa huku akiwataka wafuasi wake kuwa watulivu.

Amesema atajihusisha na mambo mapya ambayo hakutaja na kuweka wazi kwamba hatasalia kimya, na kwamba hatamchokoza yeyote.