array(0) { } Radio Maisha | Matiang'i ahudhuria kongamano la usalama Mombasa

Matiang'i ahudhuria kongamano la usalama Mombasa

Matiang'i ahudhuria kongamano la usalama Mombasa

Waziri wa Usalama wa Ndani ya Nchi Dakta, Fred Matiang'i amewasili katika kongamano la siku mbili la Wakuu wa Vitengo mbalimbali vya Idara ya Usalama linaloanza rasmi leo katika Mkahawa wa Whitesands jijini Mombasa.

Matiang'i ambaye ameandamana na Katibu wa Wizara hiyo Keriako Tobiko na Inspekta Mkuu wa Polisi Hilary Mutyambai ameratibiwa kulifungua rasmi kongamano hilo.

Baadhi ya masuala ambayo yanatarajiwa kuzungumziwa na Matiang'i ni mikakati ya kuimarishaji  usalama hasa kwenye Kaunti za Lamu na Garissa ambako katika siku za hivi karibuni yamekumbwa na mashambulio ya Al Shabab.

Jengine ni kuhusu suala la walanguzi wa mihadarati ambalo  limeathiri baadhi ya sehemu za Pwani.

Masuala ya kutathmini sera za usalama vilevile ajenda za maendeleo kwenye Idara hiyo pia yanatarajiwa kujadiliwa wakati wa kongamano hilo.

Ijumaa wiki hii wakuu hao wanatarajiwa kukutana na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Mombasa.