array(0) { } Radio Maisha | Kiunjuri asema mikakati ya kuwakabili nzige inaendelea

Kiunjuri asema mikakati ya kuwakabili nzige inaendelea

Kiunjuri asema mikakati ya kuwakabili nzige inaendelea

Waziri wa Kilimo, Mwangi Kiunjuri amesema wakati mwafaka wa kuwanyunyizia dawa nzige wa jangwani wanaoleta madhara ni wanapokuwa wametulia wakati wa usiku na mapema asubuhi.

Kiunjuri amesema hayo akisistiza kuwa mpango huo utafanikiwa kwa ushirikiano na machifu na viongozi wa jamii.

Vilevile Kiunjiru amesema mikakati ya uhamasisho inaendelea kuwekwa huku magavana wa launti za Isiolo, Meru, Samburu,Kitui, Garissa, Embu, Laikipia, Meru wakisubiriwa kuwasilisha majina ya wawakilishi watakaopokea mafunzo kuhusu wadudu hao.

Aidha, Kiunjuri amekana madai kuwa nzige hao walionekana maeneo ya Meru hapo jana akisema walikuwa panzi wa kawaida japo nzige hao wamefika leo hii katika eneo hilo mwendo wa saa tano.

Kuhusu masuala ya afya iwapo dawa inayonyunyizwa itakuwa na madhara ya baadaye kwa binadamu, mtaalamu wa mradi huo Stephen Njoka amesema wako makini kuhakikisha hakuna madhara ya aina yoyote akisema dawa wanayotumia imefanyiwa uchunguzi na kuwa nusu ya lita hunyunyizwa kwenye eneo la ukubwa wa ekari moja.