array(0) { } Radio Maisha | Peter Mugure asomewa mashtaka ya mauaji ya mkewe na wanawe

Peter Mugure asomewa mashtaka ya mauaji ya mkewe na wanawe

Peter Mugure asomewa mashtaka ya mauaji ya mkewe na wanawe

Peter Mwaura Mugure mshukiwa wa mauaji ya Joyce Syombua na wanawe wawili Shaniz Maua na Prince Michael leo hii amesomewa mashtaka ya mauaji hayo katika Mahakama ya Nyeri huku akieleza mahakama hiyo kuwa hangeweza kukubali au kuyakataa mashtaka hayo kwa sasa.

Mahakama hiyo ikiongozwa na Hakimu Jairu Ngaah imemsomea mashtaka matatu ya mauaji yaliyofanyika tarehe ishirini na sita Octoba mwaka uliopita.

Hata hivyo,  mshukiwa huyo amekosa kukiri au kukana mashtaka hayo huku akieleza mahakama kuwa angetaka mambo kadhaa kushughulikiwa.

Kwa upande wake, wakili wa Mugure Kimani Njuguna ameiomba mahakama kuskiza malalamishi ya mshukiwa wakati wa kuendelea kwa kesi hiyo.

Hapo awali kesi hiyo ilisitishwa kwa kuwa Wakili Cliff Ombeta ambaye alikuwa awakilishe Mugure alikosa kuhudhuria kesi hiyo hivyo familia ya mshukiwa kumtafuta wakili mbadala. Kesi hiyo itaanza kusikizwa tarehe ishirini na tatu mwezi huu.