array(0) { } Radio Maisha | Mahakama yamtaka Mwanasheria Mkuu kutoa maelezo ya kutoruhusiwa kwa Miguna kurejea nchini
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mahakama yamtaka Mwanasheria Mkuu kutoa maelezo ya kutoruhusiwa kwa Miguna kurejea nchini

Mahakama yamtaka Mwanasheria Mkuu kutoa maelezo ya kutoruhusiwa kwa Miguna kurejea nchini

Mahakama imemwagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Paul Kihara kujiwasilisha mbele yake siku ya Jumatatu wiki ijayo kutoa maelezo kuhusu sababu za kutoheshimiwa kwa maagizo ya mahakama ya kumruhusu wakili Miguna Miguna kurejea nchini. Jaji John Mativo amesema ni jambo la kusikitisha kwa serikali kuendelea kukiuka peupe maagizo ya mahakama.

Jaji Mativo aidha ameelezea umuhimu wa kuheshimiwa kwa maagizo ya mahakama jinsi ilivyoamrisha katiba kwa ajili ya kutendeka kwa haki katika kesi mbalimbali.

Tayari Miguna kupitia kwa wakili wake Johna Khaminwa amewasilisha waraka mahakamani kuhusu matakwa anayotaka yatimizwe. Miongoni mwa matakwa hayo ni kuamrishwa kwa serikali kutekeleza maagizo ya kumruhusu arejee na kumlipa fidia yote ambayo mahakama iliagiza alipwe.

Miguna aidha ameitaka mahakama kuishurutisha serikali kumnunulia tiketi za ndege pamoja na za mawakili wake wawili ambao watasafiri hadi aliko ili kuandamana naye atakaporejea nchini. Aidha ameitaka serikali kutompa mashatri mapya kuhusu kurejea kwake nchini na iwapo itafanya hivyo basi wahusika wahukumiwe kifungo kisichozidi miaka mitatu jela.

Miguna aliwasilisha waraka uliokuwa na maelezo kuhusu namna alivyozuiliwa kusafiri na Shirika la Ndege la Lufthansa la Ujerumani likisema lilipokea maagizo kutoka kwa serikali ya Kenya.  Ikumbukwe tayari shirika hilo limemwomba Miguna msamaha japo ametishia kulishtaki na wote waliotatiza safari yake.