array(0) { } Radio Maisha | Mbunge Moses Kuria akamatwa kwa tuhuma za kumpiga mwanamke mmoja Nairobi

Mbunge Moses Kuria akamatwa kwa tuhuma za kumpiga mwanamke mmoja Nairobi

Mbunge Moses Kuria akamatwa kwa tuhuma za kumpiga mwanamke mmoja Nairobi

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amekamatwa na maafisa wa polisi kufuatia tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mwanamke mmoja kwa jina Joyce Wanja ambaye anaarifiwa kuwa mfanyakazi wa Idhaa ya Inooro.

Wanja anadai kwamba alichapwa na Kuria tarehe 8 mwezi uliopita katika majengo ya Royal Media jijini Nairobi. Aidha, anadai kwamba polisi hawakuchukua hatua yoyote baada ya kurekodi taarifa katika Idara ya usalama.

Kwa zaidi ya saa tatu sasa, alama ya reli #ArrestMosesKuria imekuwa ikitawala mtandao wa Twitter huku wachangiaji wakiwashinikiza polisi kumkamata na kumfungulia mashtaka.