array(0) { } Radio Maisha | UASU yatoa ilani ya mgomo kufuatia mzozo kuhusu marupurupu yake
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

UASU yatoa ilani ya mgomo kufuatia mzozo kuhusu marupurupu yake

UASU yatoa ilani ya mgomo kufuatia mzozo kuhusu marupurupu yake

Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu UASU, umetoa ilani ya mgomo wa wiki moja kuhusu mzozo wa marupurupu ya shilingi bilioni 8. 8.

Uongozi wa UASU umeafikia uamuzi huo unaolenga kusambaratisha shughuli za masomo kuanzia Januari 20 katika vyuo vyote vikuu nchini.

Hatua hii inafuatia mkutano wa Kitaifa wa Wanachama wa UASU Desemba mwaka uliopita, ulioafikia kuitisha mgomo mwaka huu.

Mwenyekiti wa UASU Muga K’Olale, amesema serikali ilipuuza Mkataba wa Maelewano wa Oktoba 29 mwaka uliopita wa nyongeza ya asilimia kati ya 23.14 na 25. 07 kwa muda wa miaka minne.

Muga aidha amesema kuwa wafanyakazi wanastahili nyongeza ya asilimia 5.75 na 6.27 kila mwaka kwa mujibu wa mkataba huo.Amesema iwapo serikali haitatekeleza mkataba huo chini ya siku saba, basi shughuli za masomo zitasitishwa vyuoni.

Katibu Mkuu wa UASU Constantine Wasonga, amesema serikali imeshindwa kutekeleza mkataba huo kufikia Novemba mwaka uliopita kuendana na maelewano baina yao. Wasonga amehusisha Tume ya Kuratibu Mishahara  za Wafanyakazi SRC na Tume ya Huduma za Walimu TSC na masaibu yanaowakumba wafanyakazi wa vyuo.