array(0) { } Radio Maisha | NHIF yatangaza mabadiliko kadhaa katika utoaji wa huduma kwa wateja
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

NHIF yatangaza mabadiliko kadhaa katika utoaji wa huduma kwa wateja

NHIF yatangaza mabadiliko kadhaa katika utoaji wa huduma kwa wateja

Katika hatua ambayo inatarajiwa kuibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya, Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya, NHIF imetangaza mabadiliko kadhaa chini ya bima hiyo kukiwamo kupunguzwa kwa idadi ya watoto wanaonufaika na kadi ya wazazi wao kutoka kumi hadi watoto watano.

Mabadiliko hayo ambayo yalianza kutekelezwa tarehe mosi mwezi huu aidha yanamwidhinisha mke mmoja tu kunufaika na huduma za afya chini ya kadi moja.

Uamuzi huo uliafikiwa katika kikao maalum cha bodi ya NHIF tarehe 17 mwezi Desemba mwaka uliopita ambapo iliafikiwa kwamba iwapo familia itakuwa na watoto sita na zaidi, watano tu ndio watakaonufaika na bima hiyo huku waliosalia wakitakiwa kuongeza kiwango cha fedha wanazolipa kila mwezi.

Aidha, wanaokosa kulipa ada ya kila mwezi kwa kipindi cha miezi 12, uwanachama wao utafutiliwa mbali na kutakiwa kujisajili upya, hali inayomaanisha kwamba ataweza kuanza kunufaika na huduma hizo baada ya siku 90 baada ya kujisajili upya.

Vilevile, anayejisajili upya baada ya kukosa kulipa kwa muda uliotolewa, atalazimika kulipia ada inayotozwa kila mwezi ya shilingi mia tano kwa kipindi cha mwaka mmoja mfululizo kabla ya kuanza kutumia kadi yake.