array(0) { } Radio Maisha | Wakenya washauriwa kuwageuza kuwa kitoweo Nzige wanaoleta madhara
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakenya washauriwa kuwageuza kuwa kitoweo Nzige wanaoleta madhara

Wakenya washauriwa kuwageuza kuwa kitoweo Nzige wanaoleta madhara

Wataalamu wa masuala ya wadudu nchini wamesistiza kuwa njia mwafaka ya kuwakabili Nzige wa jangwani ni Serikali kushirikiana na serikali za kaunti kutambua maeneo ambayo yamechochea kuzaana kwa nzige hao.

Mtaalam Mary Gikungu alisema tatizo kuu lililosababisha Nzige hao kusambaa kutoka Ethiopia, Somalia hadi nchini Kenya ni ukosefu wa ushirikiano kati ya mataifa hayo, akisistiza kuwapo kwa mbinu mwafaka za kufanya utafiti ili kuzuia kusambaa  kwa wadudu hao.

Vilevile Gikungu alisema kuwa kando na kutambua maeneo ambayo yamechochea kuzaana kwa nzige hao, kuna kemikali inayonuka kama Nzige wakike inayotumiwa kuwavutia wakiume kisha kuwaua.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa Wadudu nchini, Mugo Kasinai ametoa wito kwa Wakenya walioathirika na Nzige wa Jangwani kuwageuza wadudu hao kuwa kitoweo, ila tu wahakikishe wasile walionyunyiziwa dawa.

Waatalamu hao waliofanya kikao na wanahabari katika Makavazi ya Nairobi siku ya Ahamisi walisema kuwa walitoa onyo kwa serikali mwezi Februari mwaka jana, wakati kulikiwa na dalili za nzige hao kuingia katika mataifa ya Afrika.Mtaalamu George Ong'amo ameeleza kuwa nzige hao wameingia nchini kufuatia mvua kubwa iliyoshuhudiwa mwaka jana.

Alisema nzige hao husambazwa na upepo hivyo hupeperuka zaidi ya kilomita 150. Vilevile alieleza kuwa wadudu hao huitwa Nzige wa Jangwani, kwani mara nyingi hupatikana jangwani kabla ya msimu wa mvua.

Vilevile Wataalam hao walieleza kuwa tofauti kati ya Nzige na Panzi ni kuwa Panzi wana mstari mweupe mgongoni.