array(0) { } Radio Maisha | Malkia Striker's warajea baada ya miaka kumi na sita.

Malkia Striker's warajea baada ya miaka kumi na sita.

Malkia Striker's warajea baada ya miaka kumi na sita.

Timu ya taifa ya voliboli upande wa kina dada Malkia Strikers,  imefuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki Jijini Tokyo Japan baada ya miaka kumi na Sita, mashindano ambayo yameratibiwa kuanza rasmi Julai tarehe Ishirini na nne mwaka huu na kukamilika tarehe tisa Agosti.

Malkia ambao walishiriki mashindano hayo kwa mara ya mwisho mwaka 2004, wameandikisha ushindi wao wa mwisho dhidi ya Nigeria baada ya kuwatandika seti tatu bila jibu.

Katika Seti ya kwanza , Malkia walizoa alama Ishirini na tano kwa kumi na tano, Seti ya pili Nigeria wakijikaza na kuwatatiza vipusa wa Paul Bitok licha ya kuzoa alama  Ishirini na tano kwa ishirini na moja wakimaliza seti ya tatu kwa alama Ishirini na moja kwa alama tisa.

Kumbuka Malkia chini ya kocha Paul Bitok, waliandikisha ushindi katika mechi zao zote, baada ya kuwatandika misri seti tatu kwa moja kabla ya kuwanyuka wenyeji Cameroon seti tatu kwa mbili na baadae kuwatandika Botswana seti tatu bila jibu.