array(0) { } Radio Maisha | KUPPET yakshif vikali uteketezaji wa mwalimu kitui
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KUPPET yakshif vikali uteketezaji wa mwalimu kitui

KUPPET yakshif vikali uteketezaji wa mwalimu kitui

Mauji ya mwalimu wa Shule ya msingi ya Ndooni yamekashifiwa vikali na Wakenya na washikadau katika sekta ya elimu wa hivi punde wakiwa Viongozi wa Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri, KUPPET.

Viongozi hao wamekashifu vikali mauaji ya mwalimu Daisy Mbalukhe Mbithe yaliyofanyika Siku ya Jumatatu baada ya kukatwa kwa upanga kabla ya kuteketezwa na wazazi hao walio lalamikia matokeo duni ya mtihani wa KCPE.

Katibu Mkuu wa KUPPET Akelo Misori ametoa wito kwa Waziri wa Elimu Prof. George Magoha kufunga shule hiyo mara moja kufutia hofu ya walimu, vilevile kutoa wito kwa Tume ya Huduma za Walimu TSC kuwaondoa walimu katika shule hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa KUPPET Omboko Milemba amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Upelelzi DCI, George Kinoti kufanya uchunguzi kisha kuwakamata waliohusika.

Vilevile viongozi hao wametoa wito kwa wazazi kutovamia walimu au shule, wanafunzi wasipofanya vizuri katika mtihani, kwani kufikia sasa shule kadhaa zimeathirika nchini, huku walimu wakiwa na hofu ya kuvamiwa. Kando na hayo amesema walimu wanaendelea kuhangaishwa kwani kufikia sasa hawajalipwa marurupu yao baada ya shughuli ya kusahihi mitihani ya kitaifa.

Tayari wazazi wawili wametiwa mbaroni kwa kuhusishwa na mauaji ya mwalimu Daisy.