array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa Nyanza kuwaelimisha wananchi kuhusu BBI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Viongozi wa Nyanza kuwaelimisha wananchi kuhusu BBI

Viongozi wa Nyanza kuwaelimisha wananchi kuhusu BBI

Viongozi wa eneo la Nyanza wamesema mipango imekamilika ya kuwashirikisha wakazi wa eneo hilo katika mjadala wa mapendekezo ya Ripoti ya Mpango wa Upatanishi BBI.

Wakiongozwa na Gavana wa Kisumu Prof. Anyang Nyong, viongozi hao wamekariri kauli ya kuunga ushirikiano wa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga, wakisema wapo tayari kuangazia masuala yanayoathiri uongozi wa taifa hili kuanzia kesho.

Wamesema wana imani kwamba Kenyatta na Raila watafanikisha lengo la kuwaunganisha Wakenya ili kuepuka vurugu za baada ya uchaguzi.

Kesho viongozi hao watafanya kikao cha kujadili mapendekezo ya BBI katika kaunti ya Kisii, licha ya baadhi ya wakazi wa Kisii kujitokeza jana na kupinga mpango huo.

Hayo yakijiri baadhi ya wabunge wa eneo la Magharibi wamejitokeza kuunga mkono mipango ya mkutano unaopangwa na Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU Francis Atwoli.

Viongozi hao akiwamo Seneta wa Kakamega Cleophas Malala, wamesema mkutano huo utafanyika katika Uwanja wa Bukhungu, mjini Kakamega jinsi ulivyopangwa ya kupata pingamizi.

Katika kauli inayofikirika kuwalenga washirika wa naibu wa rais katika eneo la Magharibi ambao wamekuwa wakikosoa mipango ya mkutano huo wa tarehe 18 mwezi huu, Malala amesema mkutano huo utafanyika ili kuangazia masuala yanayowaathiri wakazi wa jamii hiyo.

Kauli ya Seneta Malala imejiri kufuatia kuibuka kwa migawanyiko miongoni mwa viongozi wa Jamii ya Mulembe kuhusu ajenda za kikao hicho.

Siku kadhaa zilizopita Seneta wa Busia Amos Wako alikosoa jinsi Atwoli anavyopanga mkutano huo bila kuwashirikisha viongozi wote, hivyo kusema huenda kikao hicho kikaigawanya jamii ya Magharibi hata zaidi.