array(0) { } Radio Maisha | Sonko alalamikia kufungwa kwa akaunti zake za benki akisema hali hiyo imemfanya kukosa fedha za matumizi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sonko alalamikia kufungwa kwa akaunti zake za benki akisema hali hiyo imemfanya kukosa fedha za matumizi

Sonko alalamikia kufungwa kwa akaunti zake za benki akisema hali hiyo imemfanya kukosa fedha za matumizi

Gavana wa Nairobi, Mike Sonko sasa anaishutumu Mamlaka ya urejeshaji mali zinazomilikiwa kinyume na sheria kwa kudhibiti akaunti za benki zake bila ya agizo rasmi la mahakama.

Kwa mujibu wa Sonko, mamlaka hiyo imekuwa ikitoa agizo la kudhibitiwa kwa akaunti mbalimbali za benki anazomiliki licha ya makataa ya agizo la awali la mahakama kukamilika tarehe 27 mwezi Desemba mwaka uliopita.

Kupitia wakili wake Harrison Kinyanjui, gavana huyo ambaye alizuiliwa kuingia ofisini hadi pale kesi ya ufisadi inayomwandana itakaposikilizwa na kuamuliwa, amesema kwamba kwa sasa hawezi kuimudu familia yake kifedha pamoja na kutoweza kupokea mshahara baada ya kudhibitiwa kwa akaunti zake.

Kiongozi huyo amethibitisha kwamba amearifiwa na benki tisa anazomiliki akaunti nazo zikiwemo Benki ya National, Equity, KCB na Diamond Trust kwamba wamepokea agizo la kuzidhibiti akaunti hizo kufuatia agizo la Hakimu E. Ruany tarehe 11 mwezi uliopita.