array(0) { } Radio Maisha | Viongozi Nairobi kujadili mstakabali wa uongozi wa kaunti kufuatia kesi inayomwandama Sonko

Viongozi Nairobi kujadili mstakabali wa uongozi wa kaunti kufuatia kesi inayomwandama Sonko

Viongozi Nairobi kujadili mstakabali wa uongozi wa kaunti kufuatia kesi inayomwandama Sonko

Wawakilishi wadi katika Kaunti ya Nairobi wanatarajiwa kufanya kikao maalumu leo hii kujadili mustakabali wa uongozi wa kaunti hii.

Kikao hicho kitaongozwa na Spika Beatrice Elachi na kinatarajiwa kuangazia suala la Gavana Mike Sonko kumteua Anne Kananu Mwenda kuwa naibu wake.

Aidha, huenda kikao hicho kikatibuka baada ya wawakilishi wadi wanaomuunga mkono Sonko kutofautiana na wenzao wanaompinga kufuatia uteuzi alioufanya.

Ikumbukwe wawakilishi wanaompinga wakiongozwa na Spika Elachi walisema kwamba wanasubiri mwelekeo wa Chama cha Jubilee kabla kujadili uteuzi huo.

Kwa mujibu wa Elachi, Sonko hakufuata sheria katika uteuzi wake hivyo suala hilo huenda likakosa kujadiliwa bungeni kwa sasa.

Kauli yake ilifuatia ile ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Noordin Hajji kwmaba Sonko alikiuka sheria hasa ikizingatiwa mahakama ilimzuia kutekeleza majukumu ya ugavana baada ya kuzuiwa kuingia ofisini.